MBUNGE AZZA AWATAKA WANANCHI KULINDA MIUNDOMBINU MIRADI YA MAJI, ATOA PESA KUNUNUA KOKI ZILIZOIBWA
MBUNGE AZZA AWATAKA WANANCHI KULINDA MIUNDOMBINU MIRADI YA MAJI, ATOA PESA KUNUNUA KOKI ZILIZOIBWA
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Masekelo. Na Marco Maduhu, Elizabeth Cosmas- SHINYANGA Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, amewataka wananchi wa kijiji cha Masekelo, Kata ya Bukene wilayani Shinyanga, kulinda miundombinu ya miradi ya maji ili iweze kuwahudumia kwa muda mrefu, akieleza kuwa serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kutekeleza miradi hiyo. TAZAMA VIDEO 👇👇 Azza ametoa wito huo jana, Septemba 21, 2026, wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji hicho, baada ya kubainika kuwa watu wasiojulikana wameiba koki 15 za maji na kusababisha baadhi ya wananchi kukosa huduma hiyo. Amesema serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imekuwa ikiwekeza fedha nyingi katika utekelezaji wa miradi ya maji, hivyo wananchi wanapaswa kuilinda na kutoa taarifa kwa viongozi na vyombo vya ulinzi na usalama kuhusu watu wanaohujumu miundombinu hiyo. “Ninashukuru Shule ya Msingi Masekelo wenyewe wamenunua koki saba ili wanafu…