MASAUNI ASISITIZA UTEKELEZAJI WA SIKU YA USAFI KILA MWISHO WA MWEZI
MASAUNI ASISITIZA UTEKELEZAJI WA SIKU YA USAFI KILA MWISHO WA MWEZI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akiongozana na viongozi mbalimbali kufanya usafi katika Soko la Buguruni, Jijini Dar es Salaam, Septemba 5, 2026. ************ Na; Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Serikali inatoa wito kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji kuhakikisha kuwa wanaweka utaratibu wa kusimamia utekelezaji wa maelekezo ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kuwa siku ya usafi wa Mazingira Kitaifa kwa kuzingatia maslahi ya makundi mbalimbali. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni ameyasema hayo mara baada ya kuongoza zoezi la usafi katika Soko la Buguruni Jijini Dar es Salaam, Septemba 5, 2026. “Tunakumbuka kuwa Serikali kupitia Mheshimiwa Rais akiwa Makamu wa Rais mwaka 2016 alitoa agizo kuwa kila Jumamosi ya mwisho ya mwezi kuwa siku ya usafi wa Mazingira Kitaifa. Aidha Ofisi ya Ma…