MAHAKAMA YARUHUSU LISSU KUWAITA IGP, CDF NA DCI
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imeamuru kutolewa kwa wito (summons) kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), ili kutoa ushahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu. Uamuzi huo umetolewa leo na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dustan Ndunguru baada ya Mahakama kusikiliza hoja za upande wa mashtaka na utetezi kuhusu ombi la Lissu la kuwaita mashahidi hao pamoja na viongozi wengine wa Serikali. Mahakama imesema, kwa kuzingatia kifungu cha 314 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), ina hiari ya kuruhusu mashahidi kuitwa kwa kuangalia umuhimu wa ushahidi wao katika shauri. Katika uamuzi huo, Mahakama imesema imeridhika kuwa ushahidi wa IGP, CDF na DCI ni muhimu katika kesi hiyo, hivyo imeamuru summons zitolewe ili waje kutoa ushahidi upande wa utetezi. Hata hivyo, Mahakama imekataa ombi la kuwaita baadhi ya mashahidi waliotajwa na Lissu, akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mk…