KONGAMANO LA UFUATILIAJI NA TATHMINI KUWAKUTANISHA WASHIRIKI 1,500 ARUSHA

KONGAMANO LA UFUATILIAJI NA TATHMINI KUWAKUTANISHA WASHIRIKI 1,500 ARUSHA
Vero Ignatus – Michuzi TV Arusha KONGAMANO la Kitaifa la Ufuatiliaji na Tathmini linatarajiwa kufanyika jijini Arusha kuanzia Septemba 22 hadi 26, 2026, likiwakutanisha washiriki kutoka serikalini, taasisi za umma, sekta binafsi pamoja na wadau wa maendeleo. Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla, amesema kongamano hilo litafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Ngurdoto, wilayani Arumeru, na linatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 1,500, huku mgeni rasmi akiwa Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba. Makalla amesema kongamano hilo litajadili uzoefu, ubunifu na mbinu bora za ufuatiliaji na tathmini, pamoja na namna ya kutumia matokeo ya tathmini katika kuboresha utoaji wa huduma kwa umma na kuhakikisha shughuli za maendeleo zinawanufaisha wananchi. Amesema ufuatiliaji na tathmini ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha utekelezaji wa mipango ya maendeleo unafanyika kwa ufanisi na matokeo yanayopimika, huku wananchi wakipata fursa ya kutoa ushahidi kuhusu utek…