KOMBO: WANAWAKE MUHIMU KUPATA SULUHISHO LA AMANI MASHARIKI MWA DRC

KOMBO: WANAWAKE MUHIMU KUPATA SULUHISHO LA AMANI MASHARIKI MWA DRC
Na Mwandishi Wetu, New York WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amesema ushiriki wa wanawake katika michakato ya amani ni muhimu katika kupata suluhisho endelevu kwa changamoto za usalama katika eneo la Maziwa Makuu, hususan Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Mhe. Kombo ameyasema hayo katika Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu kuendeleza Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama katika juhudi za amani eneo la Maziwa Makuu, uliofanyika pembezoni mwa Kikao cha 81 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani. Amesema hali ya usalama Mashariki mwa DRC inaendelea kuwa ya kutia wasiwasi, huku wanawake na wasichana wakikabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo kuhama makazi, ukatili wa kingono na ukosefu wa mahitaji muhimu. Kutokana na hali hiyo, Mhe. Kombo amesema Tanzania imesisitiza umuhimu wa utekelezaji wa Azimio Na. 1325 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, linalohimiza ushiriki wa wanawake …