KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YAPATIWA MAFUNZO KUHUSU MIKATABA YA MSAADA WA KIUFUNDI KATIKA SEKTA YA MADINI

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YAPATIWA MAFUNZO KUHUSU MIKATABA YA MSAADA WA KIUFUNDI KATIKA SEKTA YA MADINI
DODOMA, Septemba 3, 2026 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Subira Mgalu (Mb.) imepatiwa mafunzo kuhusu usimamizi wa mikataba ya msaada wa kiufundi katika Sekta ya Madini, ikiwa ni pamoja na masharti ya kisheria yanayohusu umiliki wa leseni ndogo za uchimbaji wa madini. Akizungumza kupitia mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Madini jijini Dodoma mapema leo Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Madini, Francis Kayichile, kwa Niaba ya Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini amesisitiza kuwa mtu ambaye si raia wa Tanzania kupewa leseni ndogo ya uchimbaji madini ni kosa kwa mujibu wa Sheria ya Madini, Sura ya 123, kwa kuwa fursa ya kuomba na kumiliki leseni hizo imetengwa kwa Watanzania pekee. Kayichile amesema Kifungu cha 64 kikisomwa pamoja na kifungu cha 9 (3) cha Sheria ya Madini, Sura ya 123, kinatoa fursa kwa Watanzania pekee kuwasilisha maombi ya leseni ndogo za uchimbaji madini, hivyo mtu asiye raia wa Tanzan…