KABLA YA PENSHENI DAIMU SALUM MKWAWA ATOA SOMO LA KUWEKEZA MAPEMA KWA AJILI YA MAISHA BAADA YA KUSTAAFU
KABLA YA PENSHENI DAIMU SALUM MKWAWA ATOA SOMO LA KUWEKEZA MAPEMA KWA AJILI YA MAISHA BAADA YA KUSTAAFU
Hii ndio Royal Woodbridge Hotel iliyojengwa na kuwekezwa na mstaafu Daim Salum Mkwawa Hotel hii ipo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma mkabala na stendi ya Seedfarm njia inayokwenda Songea-Tunduru-Lindi Muonekano wa ndani wa Hotel ya Royal Woodbridge iliyopo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma inayomilikiwa na Daimu Salum Mkwawa Hapa ni eneo la kupatia chai na chakula katika Hotel ya Royal Woodbridge iliyopo Seedfarm Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Na Regina Ndumbaro Songea-Ruvuma Kustaafu kutoka kwenye ajira hakumaanishi mwisho wa uzalishaji au mchango wa mtu katika uchumi wa nchi, bali kunaweza kuwa mwanzo wa hatua nyingine ya maisha endapo mtumishi ataandaa mapema shughuli za kiuchumi zitakazomsaidia baada ya kuondoka kazini. Hilo ni miongoni mwa masomo yanayoweza kupatikana katika safari ya Daimu Salum Mkwawa, msomi na mwanazuoni aliyewahi kufanya kazi katika taasisi mbalimbali za Serikali na baadaye kuhudumu katika Umoja wa Mataifa (UN) kwa miaka 18. Mkwawa, ambaye sasa ni mstaafu, a…