KABEKE: UISLAMU SI KUSWALI PEKE YAKE
NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA SHEIKH wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Hassan Kabeke, amesema Uislamu si dini ya kuswali, kufunga na kwenda Hijja pekee, bali ni dini inayopaswa kutumika kutatua changamoto za watu na jamii, huku akitaka Maulid zitumike kudumisha amani na kuondoa mifarakano. Alisema hayo jana jijini Mwanza, katika Maulid ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Ithna Asheriyyah Tanzania (TIC), akisisitiza kuwa waumini wanapaswa kuonyesha mafundisho ya dini kwa vitendo, hususan kuwasaidia wenye mahitaji. Sheikh Kabeke alisema mtu anayekuja kuomba msaada wa matibabu anapopewa barua ya kuchangisha fedha, mchango huo unapaswa kumsaidia kutatua tatizo lake, akisema kutoa kiasi kidogo kisichokidhi mahitaji halisi ni kinyume na dhana ya kusaidiana katika dini. “Tunaposhindwa kufanya kazi tusilete visingizio. Mnalalamika Shia wanachukua waumini wenu, ndiyo, wanafanya kazi. Haya mnayoyafanya ndugu zetu Washia yanatuamsha,” alisema. Alisema Waislamu wan…