JUKWAA LA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA WALIPAKODI (OMBUDSMAN ) LAFUNGULIWA RASMI JIJINI ARUSHA .

JUKWAA LA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA WALIPAKODI (OMBUDSMAN ) LAFUNGULIWA RASMI JIJINI ARUSHA .
Waziri wa fedha Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil akizungumza wakati wa ufunguzi wa jukwaa la kushughulikia malalamiko ya walipa kodi (ombudsman) jijini Arusha . Msuluhishi wa maswala ya kikodi ,Erastus Mtui akizungumza kwenye jukwaa hilo ………..  Happy Lazaro,Arusha . Arusha.Kuimarishwa kwa mfumo wa kushughulikia malalamiko ya walipa kodi (ombudsman) kumetajwa kuwa muhimu katika kuhakikisha wanapata haki na kujenga uwazi katika ukusanyaji wa mapato nchini. Hayo yamesemwa jijini Arusha leo na Waziri wa fedha Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil wakati wa ufunguzi wa jukwaa la kushughulikia malalamiko ya walipa kodi (ombudsman), limewakutanisha wadau mbalimbali, wakiwemo wataalamu wa masuala ya kodi kutoka ndani na nje ya nchi. Dkt.Juma amesema uwepo wa mfumo imara wa kushughulikia malalamiko ya walipa kodi (ombudsman) utasaidia walipa kodi kupata suluhisho pale wanapohisi hawajatendewa haki na taasisi za kodi. Amesema kuwa ,Jukwaa hilo kufanyika nchini Tanzania limetajwa kuwa muhimu katika kuimarisha h…