JETOUR TANZANIA YAZINDUA MAGARI MAPYA YA PLUG-IN HYBRID,YAZINGATIA UFANISI WA NISHATI
JETOUR TANZANIA YAZINDUA MAGARI MAPYA YA PLUG-IN HYBRID,YAZINGATIA UFANISI WA NISHATI
Kampuni ya JETOUR Tanzania imezindua JETOUR Club na kutambulisha magari mawili mapya yenye teknolojia ya plug-in hybrid, JETOUR G700 na JETOUR F700, hatua inayolenga kuwapa Watanzania chaguo zaidi katika matumizi ya usafiri unaozingatia ufanisi wa nishati. Uzinduzi huo unafanyika wakati dunia ikikabiliwa na changamoto za upatikanaji wa mafuta na kuongezeka kwa gharama za nishati, hali inayosukuma matumizi ya teknolojia zinazolenga kupunguza utegemezi wa mafuta. Tanzania nayo inaendelea kuchukua hatua katika kuhamasisha matumizi yenye ufanisi ya nishati na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ya mafuta, chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Kwa mujibu wa JETOUR Tanzania, magari hayo mapya yanachanganya matumizi ya umeme na mafuta, hivyo kumpa mtumiaji fursa ya kutumia umeme katika safari fupi na mafuta kwa safari ndefu, kulingana na mahitaji ya safari. Hatua hiyo inalenga kuongeza chaguo kwa Watanzania wanaohitaji magari yenye uwezo wa kufany…