ILANI YA CCM 2025–2030 NI JUMUISHI KWA MAKUNDI YOTE YA KIJAMII,ITATEKELEZWA - RABIA

ILANI YA CCM 2025–2030 NI JUMUISHI KWA MAKUNDI YOTE YA KIJAMII,ITATEKELEZWA - RABIA
TABORA, Tanzania  Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Ndg. Rabia Abdalla Hamid, amesema Ilani ya CCM ya mwaka 2025–2030 ni jumuishi na inalenga kutekeleza mahitaji na matarajio ya makundi yote ya kijamii nchini. Rabia amesema hayo leo, Septemba 25, 2026, wakati akiendelea na ziara ya CCM katika Mkoa wa Tabora yenye lengo la kusikiliza, kuzungumza na wananchi pamoja na kutafuta majawabu ya changamoto zinazowakabili. Katika ziara hiyo, Rabia amekutana na wananchi kutoka makundi mbalimbali ya kijamii ambao walipata fursa ya kuwasilisha changamoto zao na kutoa maoni kuhusu masuala yanayogusa maisha yao na maendeleo ya maeneo yao. Amesema CCM imeweka katika Ilani yake ya 2025–2030 mipango inayolenga kuhakikisha makundi yote ya kijamii yanashirikishwa na kunufaika na juhudi za Serikali katika kuleta maendeleo. “Ilani ya CCM ya 2025–2030 ni jumuishi kwa makundi yote ya kijamii. CCM itatekeleza ahadi zote ilizowaahi…