DUKA JIPYA LA YAS KUFUNGUA FURSA KWA WAKAZI WA KAHAMA

DUKA JIPYA LA YAS KUFUNGUA FURSA KWA WAKAZI WA KAHAMA
Kahama, Septemba 24, 2026 – Wakazi na wafanyabiashara wa Kahama mkoani Shinyanga wanatarajiwa kunufaika na upatikanaji wa huduma za mawasiliano na kifedha kwa urahisi zaidi, kufuatia Yas Tanzania kufungua duka jipya mjini humo. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Mhe. Mataluma Kaniki alisema kuendelea kuongezeka kwa uwekezaji wa sekta binafsi ni muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi na kuongeza fursa za ajira katika Manispaa hiyo. “Kahama ni miongoni mwa maeneo yanayokua kwa kasi kiuchumi kutokana na shughuli za madini, kilimo na biashara. Tunapopata uwekezaji kama huu, tunaona matokeo yake si katika huduma pekee, bali pia katika ajira, biashara zinazozunguka uwekezaji huo na mchango wake katika uchumi wa Manispaa yetu. Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri yatakayovutia uwekezaji zaidi Kahama,” alisema Mhe. Kaniki. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Uendeshaji wa Yas Tanzania, Bi. Mwangaza Matotola, a…