DKT. SAMIZI AKABIDHI VIFAA VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 87 MUHAMBWЕ

DKT. SAMIZI AKABIDHI VIFAA VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 87 MUHAMBWЕ
Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Muhambwe, Dkt. Florence Samizi, amekabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 87 katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Muhambwe, Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Mkoa wa Kigoma, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi alizozitoa wakati wa kampeni. Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na mabati 1,050 yenye thamani ya Shilingi milioni 37, saruji mifuko 289 yenye thamani ya Shilingi milioni 6.936, pamoja na kompyuta na printa moja vyenye thamani ya Shilingi milioni 3.5. Aidha, Dkt. Samizi ametoa zaidi ya Shilingi milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa vivuli katika maeneo ya masoko, hatua inayolenga kuboresha mazingira ya wafanyabiashara na wananchi wanaotumia masoko hayo. Dkt. Samizi amekabidhi vifaa hivyo akiwa katika ziara ya jimboni kwake, ikiwa ni sehemu ya kuendelea kuwashukuru wananchi kwa ushirikiano wao pamoja na kutekeleza ahadi alizozitoa wakati wa kampeni. Katika ziara hiyo, Dkt. Samizi amewaasa wananchi kuendelea kutumi…