DKT. SAJAD RAI KUIBEBA TANZANIA 'WORLD CEO SUMMIT 2026 AFRICA'
DKT. SAJAD RAI KUIBEBA TANZANIA 'WORLD CEO SUMMIT 2026 AFRICA'
MTAALAM katika Sekta ya Nishati ya Mafuta nchini Dkt. Sajad Habib Rai, ameteuliwa kuwa mjumbe na mmoja wa wazungumzaji mashuhuri(Jopo) katika Mkutano wa 'World CEO Summit 2026 Africa' unaotarajiwa kufanyika Novemba 26 hadi 27 Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo wa kimkakati utakaojadili kuhusu masuala ya uwekezaji sambamba na mahusiano ya kibiashara kwa siku hizi mbili, utawakutanisha zaidi ya Wakurugenzi Wakuu (CEOs) 1,000, Wawekezaji, watunga Sera na viongozi wa sekta mbalimbali kutoka zaidi ya nchi 50. Dkt Sajad Habib Rai ambaye ni Meneja Mkazi wa 'Mansoor Industries Limited', anatarajiwa kuzungumza katika Mkutano huo juu ya uzoefu wake kuhusu masuala ya maendeleo ya viwanda, nishati, uwekezaji, uendelevu na ushirikiano wa kimkakati kwa ajili ya kukuza uchumi wa Afrika. "Dkt. Rai atatoa mitazamo na uzoefu muhimu kuhusu maendeleo ya viwanda, nishati, uendelevu, uwekezaji, pamoja na ushirikiano wa kimkakati unaohitajika ili kuimarisha uwezo wa uzalishaji barani Afrik…