DKT. MWIGULU: UWEZESHAJI WA WANAWAKE NI UWEKEZAJI KATIKA AFYA MOJA
DKT. MWIGULU: UWEZESHAJI WA WANAWAKE NI UWEKEZAJI KATIKA AFYA MOJA
▪️︎ Aeleza hatua za Tanzania kuwawezesha wanawake katika kilimo WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba alisema uwezeshaji wa wanawake wakulima ni uwekezaji katika utekelezaji wa dhana ya Afya Moja, kutokana na nafasi yao katika uzalishaji wa chakula, ufugaji, lishe, afya ya mifugo, usalama wa chakula na utunzaji wa mazingira. “Wanawake hawapo pembezoni mwa mifumo ya chakula na kilimo; wako katikati yake. Kuwawezesha wanawake ni uwekezaji si katika kilimo pekee, bali pia katika Afya Moja,” alisema. Waziri Mkuu alisema hayo jana (Jumatatu, Septemba 21, 2026) wakati akizungumza katika kikao cha ngazi ya juu kuhusu Mwaka wa Kimataifa wa Mwanamke Mkulima 2026, chenye mtazamo wa Afya Moja, kilichofanyika katika Kituo cha Sheikh Zayed, Makao Makuu ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), jijini Roma, Italia. Alisema Tanzania inaongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ni Rais wa kwanza mwanamke katika historia ya nchi, akieleza kuwa wanawake wana nafasi kubwa katika uzalisha…