DKT. MWIGULU: KILA KIJIJI KUWA NA SEKONDARI

DKT. MWIGULU: KILA KIJIJI KUWA NA SEKONDARI
▪️︎ Aelekeza fedha zinazookolewa kwenye kubana matumizi zielekezwe kwenye huduma za wananchi ▪️︎ Aagiza magari ya kubeba wagonjwa yawe na mafuta, aonya wanaowachangisha wagonjwa ▪️︎ Ampongeza Afisa Elimu aliyesimamia shule kuongoza kitaifa WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali imejipanga kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu, ikiwemo kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na shule ya sekondari, na zaidi ya vyumba 16,000 vya madarasa vikitarajiwa kujengwa ili kukidhi ongezeko la wanafunzi. Dkt. Mwigulu amesema hayo leo, Jumamosi, Septemba 05, 2026, wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma, katika Viwanja vya Halmashauri ya Bahi, alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kuwasikiliza wananchi na kushughulikia changamoto zinazowakabili. Amesema uamuzi wa kuongeza muda wa elimu ya lazima hadi kidato cha nne unaleta mahitaji makubwa ya miundombinu ya elimu, yakiwemo madarasa, maabara na maktaba. “Tunaposema elimu ya laz…