DKT. MWIGULU ATOA WITO WA MAANDALIZI YA MAPEMA KUKABILI ATHARI ZA EL NIÑO
DKT. MWIGULU ATOA WITO WA MAANDALIZI YA MAPEMA KUKABILI ATHARI ZA EL NIÑO Atoa rai kwa Watanzania kuchukua tahadhari dhidi ya mafuriko Aagiza ndani ya Septemba kutangazwa zabuni ya ujenzi wa barabara km 11 za Igauri–Ilongero WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ametoa wito kwa Watanzania na viongozi katika ngazi zote kuchukua tahadhari na kujiandaa mapema kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua kubwa zinazohusishwa na hali ya El Niño. Dkt. Mwigulu ametoa rai hiyo leo, Jumapili, Septemba 06, 2026, wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la Ilongero, Wilaya ya Singida, mkoani Singida, katika ziara yake ya kikazi ya kusikiliza kero za wananchi na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Amesema maeneo yenye historia ya mafuriko yanapaswa kutambuliwa mapema na hatua za tahadhari kuchukuliwa, huku akiwataka wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi kuzingatia taarifa na maelekezo ya mamlaka husika. “Maeneo ambayo mnaona ni ya hatari sana Watanzania tunayajua. Tunayajua maeneo yenye historia ya mafuriko. Ni vyema tukaanza kuchukua tahadhari kw…