DKT. MWIGULU ATETA NA MKURUGENZI MKUU WA FAO

DKT. MWIGULU ATETA NA MKURUGENZI MKUU WA FAO
*Ataja umwagiliaji, zana za kisasa za kilimo, na uongezaji thamani kuwa maeneo ya kimkakati WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imedhamiria kuongeza uwekezaji katika maeneo ya umwagiliaji, uzalishaji wa mbegu kwa wingi na matumizi ya zana za kilimo kisasa kama njia ya kuimarisha sekta ya kilimo. Amesema hayo leo (Jumatatu, Septemba 21, 2026) wakati akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Dkt. Qu Dongyu kuhusu mageuzi ya mifumo ya chakula na kilimo nchini Tanzania, ambako anashiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kujadili Afya Moja na Mifumo ya Chakula na Kilimo unaofanyika katika Makao Makuu ya FAO, jijini Roma, Italia. Dkt. Mwigulu amesema Serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeongeza uwekezaji katika kilimo na kuelekeza nguvu katika miradi ya kimkakati, huku ikilenga kuhakikisha wakulima wanapata zana za kilimo na huduma bora zaidi katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Amesema Tanzania pia ina fursa kubwa …