DKT. MWIGULU AAGIZA MFUMO MPYA WA UNUNUZI PAMBA UWE TAYARI NDANI YA MWEZI MMOJA
DKT. MWIGULU AAGIZA MFUMO MPYA WA UNUNUZI PAMBA UWE TAYARI NDANI YA MWEZI MMOJA
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amemuagiza Waziri wa Kilimo kukutana na wadau wa zao la pamba na ndani ya mwezi mmoja kuwasilisha mapendekezo ya mfumo bora wa ununuzi wa pamba utakaowanufaisha wakulima na kuchochea uzalishaji wa zao hilo nchini. Dkt. Mwigulu ametoa agizo hilo leo, Jumatatu Septemba 14, 2026, wakati akizungumza na wananchi wa Itilima mkoani Simiyu, baada ya Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu Daudi Silanga, kuwasilisha changamoto zinazowakabili wakulima wa pamba, ikiwemo malalamiko kuhusu mfumo wa sasa wa ununuzi wa zao hilo. “Leo tarehe 14, mpaka tunapofika tarehe 14 mwezi ujao, niwe nimeshapata taarifa ya utaratibu mzuri ambao tutakubaliana,” amesema Dkt. Mwigulu. Amesema Serikali italinganisha mifumo iliyowahi kutumika katika ununuzi wa pamba na mfumo unaotumika sasa, ili kubaini utaratibu utakaokuwa na manufaa zaidi kwa wakulima, huku ukilinda uzalishaji, bei ya pamba na maisha ya wananchi wanaotegemea zao hilo. Akizungumzia masuala mengine yanayowagusa wananchi, Dkt. Mwi…