DKT. MDAKU: ZIARA YA MAFUNZO CHINA YATOA SOMO LA KUENZI HISTORIA YA TANZANIA

DKT. MDAKU: ZIARA YA MAFUNZO CHINA YATOA SOMO LA KUENZI HISTORIA YA TANZANIA
Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Mhe. Dkt. Mecktridis Mdaku, ameendelea na ziara ya mafunzo nchini China kwa kutembelea makumbusho na maeneo ya kihistoria na kiutamaduni, akijifunza namna nchi hiyo inavyohifadhi na kuenzi historia, mila na utamaduni wake. Katika ziara hiyo, Mhe. Dkt. Mdaku ametembelea eneo la kihistoria na kiutamaduni la Old Street, ambako amejifunza kuhusu utamaduni wa majengo ya kale, historia ya Barabara ya Kale ya Hariri ya Baharini, utamaduni wa ufinyanzi wa Ni Xing Tao pamoja na tamaduni nyingine zilizohifadhiwa na kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Ziara hiyo imempa Dkt. Mdaku fursa ya kujionea namna China inavyotumia makumbusho kuhifadhi historia na utamaduni wake, huku ikihakikisha vizazi vipya vinaendelea kuifahamu na kuthamini historia ya waliowatangulia. Akibeba somo hilo, amesema Tanzania pia ina utajiri mkubwa wa historia na urithi unaopaswa kutunzwa, kuendelezwa na kufikishwa kwa vizazi vijavyo. “Nimeona namna wanavyothamini historia yao na kuhakikis…