DIGITAL TANZANIA YABADILI MFUMO WA HUDUMA ZA SERIKALI
DIGITAL TANZANIA YABADILI MFUMO WA HUDUMA ZA SERIKALI Na Sophia Kingimali, Dar es Salaam MRADI wa Digital Tanzania umewezesha kuboresha mawasiliano ya kimtandao na upatikanaji wa huduma za Serikali kwa njia ya kielektroniki, huku Serikali ikieleza kuwa utekelezaji wake umeleta mafanikio katika maeneo mbalimbali ikiwemo miundombinu, mifumo ya kidijitali na ujenzi wa uwezo. Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 14,2026 Jijini Dar es salaam wakati wa tathmini ya utekelezaji wa mradi huo, Mkurugenzi wa TEHAMA Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Priscus Kiwango, amesema mradi huo umekuwa na mchango mkubwa katika kuongeza upatikanaji wa mawasiliano, hasa maeneo ya vijijini yaliyokuwa na changamoto ya huduma hiyo. Amesema kupitia mradi huo, minara ya mawasiliano imejengwa katika maeneo mbalimbali ambayo awali hayakuwa na mawasiliano, huku teknolojia ikiboreshwa hadi kufikia 3G na 4G, hatua inayowawezesha wananchi kutumia intaneti na huduma mbalimbali za kidijitali. Kwa mujibu wa Kiwango, mradi umewezesha pia ta…