DCP DKT MAMBOSASA AMWAKILISHA IGP KUWAAGA MAAFISA, WAKAGUZI NA ASKARI WANAOKWENDA MAFUNZO NCHINI INDONESIA.

DCP DKT MAMBOSASA AMWAKILISHA IGP KUWAAGA MAAFISA, WAKAGUZI NA ASKARI WANAOKWENDA MAFUNZO NCHINI INDONESIA.
Na. Jeshi la Polisi Dar es Salaam. Katika kuhakikisha Jeshi la Polisi linaaendelea kujiimarisha katika Mafunzo na kutoa huduma Bora kwa Wananchi limeendelea kutoa mafunzo ndani na nje ya Tanzania kwa lengo la kuwajengea uwezo askari katika kutekeleza majukum kwa weledi na usasa ili kufanikisha adhima ya kutoa huduma bora kwa wananchi wanaolitegemea Jeshi hilo kwa ulinzi wao na mali. Akiwaaga kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Camillus Wambura Mkuu wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Dkt Lazaro Mambosasa  amewataka Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali wanaokwenda kuhudhuria mafunzo nchini Indonesia, kutumia vyema fursa hiyo kwa kuzingatia masomo watakayopatiwa na kuhakikisha maarifa na ujuzi watakaoupata unakuwa chachu ya kuleta tija, ufanisi na usasa katika utendaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, hususani katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi. Ameongeza kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi amesisitiza  washiriki hao wanataki…