CRDB NA TRA SACCOS WAPIGA HATUA KIDIJITALI KWA PESACARD

CRDB NA TRA SACCOS WAPIGA HATUA KIDIJITALI KWA PESACARD
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam, 5 Septemba 2026 – Benki ya CRDB kwa kushirikiana na TRA SACCOS imezindua rasmi TRA SACCOS PESACARD, kadi mpya inayotumia mfumo wa Visa inayolenga kuwapa wanachama wa TRA SACCOS urahisi, uhuru na wigo mpana zaidi wa kupata na kutumia fedha zao, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 ya TRA SACCOS. Uzinduzi huo ni hatua muhimu katika ushirikiano wa muda mrefu kati ya Benki ya CRDB na TRA SACCOS, na unaashiria awamu mpya ya mageuzi ya kidijitali katika utoaji wa huduma za kifedha kwa wanachama wa SACCOS hiyo. Kupitia TRA SACCOS PESACARD, wanachama wataunganishwa na mfumo mpana wa malipo wa Visa na hivyo kuwa na uwezo wa kutoa fedha kupitia ATM pamoja na kufanya malipo katika vituo vya POS vinavyokubali Visa ndani na nje ya Tanzania. Akizungumza katika maadhimisho hayo, Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo aliipongeza TRA SACCOS kwa kufikisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwake, huku akiipongeza Benki ya CRDB kwa kuendelea kutumia uwezo wake wa kiteknoloj…