CCM KISHAPU YASIKILIZA KERO ZA WAFUGAJI MWAMALASA YAAHIDI SERIKALI KUZITATUA
CCM KISHAPU YASIKILIZA KERO ZA WAFUGAJI MWAMALASA YAAHIDI SERIKALI KUZITATUA
Na Sumai Salum-Kishapu Wananchi na wafugaji wa Kata ya Mwamalasa wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga, wameeleza changamoto mbalimbali zinazowakabili, ikiwemo upatikanaji wa maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu na mifugo, huku wakiiomba Serikali kuongeza matanki ya kuhifadhi maji na kuchimba visima. Akizungumza katika kikao cha viongozi wa CCM Wilaya ya Kishapu kilichofika katika kata hiyo leo Septemba 20, 2026, Matu Kidai amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuboresha huduma za kijamii, akitaja ujenzi na uboreshaji wa barabara pamoja na kufikishwa kwa umeme katika maeneo ya wananchi. Naye Katibu wa Kikundi cha Wafugaji Miyuguyu, Majeshi Buyaye, amesema maji yanayopatikana kupitia matanki yaliyopo hayatoshi mahitaji ya wananchi na mifugo, hivyo ameomba kuongezwa kwa matanki pamoja na kuchimbwa kwa visima ili kuongeza upatikanaji wa maji. Mwenyekiti wa wafugaji Kata ya Mwamalasa, Makoye Kachemba amepongeza juhudi za viongozi wa CCM na Serikali kufika katika kata hiyo kusikiliz…