BUNGE LARIDHIA MKATABA UANZISHWAJI TAASISI YA UKUZAJI MAENDELEO YA KIJANI

BUNGE LARIDHIA MKATABA UANZISHWAJI TAASISI YA UKUZAJI MAENDELEO YA KIJANI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akiwasilisha maelezo kuhusu azimio la kuridhia Mkataba wa Uanzishwaji wa Taasisi ya Ukuzaji wa Maendeleo ya Kijani Duniani, bungeni jijini Dodoma leo Septemba 03, 2026. Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa (kulia) akishiriki kikao cha Bunge jijini Dodoma leo Septemba 03, 2026. Wengine ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. James Milya na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mshamu Munde  Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Maduhu Kazi (katika) akifuatilia kikao cha Bunge jijini Dodoma leo Septemba 03, 2026. Katika kikao hicho Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni aliwasilisha maelezo kuhusu Azimio la kuridhia Mkataba wa Uanzishwaji wa Taasisi ya Ukuzaji wa Maendeleo ya Kijani Duniani. Wengine pichani ni Wakurugenzi Wasaidizi Idara ya Mazingir…