BUNGE LAPITISHA MUSWADA WA SHERIA NA 2 WA MWAKA 2026
BUNGE LAPITISHA MUSWADA WA SHERIA NA 2 WA MWAKA 2026 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 2) wa Mwaka 2026 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 02) Bill, 2026), tarehe 2 Septemba, 2026 katika Mkutano wa Nne, Kikao cha Sita cha Bunge kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma. Akizungumza wakati wa kuwasilisha Muswada huo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari amesema kuwa Muswada unakusudia kufanya maboresho katika Sheria kuu Saba. *”Malengo ya marekebisho haya ni kuboresha utekelezaji wa masharti ya sheria husika na kuzifanya sheria hizi ziendane na wakati na kuleta tija kwa wananchi.”* Amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali Aidha, Mwanasheria Mkuu amezitaja Sheria zilizofanyiwa marekebisho ni pamoja na Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi, Sura ya 116, Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287, Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji), Sura ya 288 na Sheria ya Baraza la Usalama la Taifa, Sura ya 61. Mhe. Johari ameendelea …