BARAZA LA TAIFA LA WATOTO LAOMBA KUKUTANA NA RAIS SAMIA

BARAZA LA TAIFA LA WATOTO LAOMBA KUKUTANA NA RAIS SAMIA
Na Dotto Kwilasa,Dodoma Baraza la Taifa la Watoto limeomba kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan ili kuwasilisha mapendekezo na changamoto zinazohusu ustawi, ulinzi na maendeleo ya watoto nchini. Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watoto, Daniel Magembe, wakati wa uzinduzi wa Kanuni za Uanzishaji, Uendeshaji na Uratibu wa Mabaraza ya Watoto nchini, jijini Dodoma leo Septemba 11, 2026. Magembe amesema kikao hicho kitatoa fursa kwa Baraza kuwasilisha kwa Rais masuala mbalimbali yanayowahusu watoto, yakiwemo maboresho ya Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, hususan suala la umri wa kuolewa, pamoja na mahitaji ya kuboresha miundombinu inayotumika katika shughuli za watoto. Amesema Baraza la Watoto kupitia Kamati Kuu limejadili mapendekezo mbalimbali yanayolenga kuimarisha ulinzi na ustawi wa watoto, hivyo ni muhimu mapendekezo hayo yawasilishwe katika ngazi ya juu ya Serikali. Kwa upande mwingine Magembe ameishukuru Serikali kwa hatua ya kuhakikisha Mabaraza ya Watoto yanatambuli…