AZZA AAHIDI KUTOA MIFUKO YA SARUJI, MABATI NA MBAO UKAMILISHAJI NYUMBA ZA WATUMISHI NGOKOLO NA IGEMBYA ZIARA YA KIJIJI KWA KIJIJI

AZZA AAHIDI KUTOA MIFUKO YA SARUJI, MABATI NA MBAO UKAMILISHAJI NYUMBA ZA WATUMISHI NGOKOLO NA IGEMBYA ZIARA YA KIJIJI KWA KIJIJI
Na Marco Maduhu, Elizabeth Cosmas, SHINYANGA Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad, ameahidi kutoa mifuko 150 ya saruji kwa ajili ya kuanzishwa kwa ujenzi wa nyumba ya Mganga katika Zahanati ya Ngokolo Kata ya Tinde, wilayani Shinyanga, ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya muda wote, hasa kwa wagonjwa wa dharura nyakati za usiku. TAZAMA VIDEO 👇👇 Pia, ameahidi pia kutoa bati 46, mbao 50 na mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa nyumba ya walimu katika shule ya msingi Itubanilo Kijiji cha Igembya ambayo ipo katika hatua ya ukamilishaji. Ahadi hizo amezitoa leo Septemba 23, 2026, kwa nyakati tofauti wakati, alipofanya ziara katika vijiji vya Ngokolo na Igembya, kwa ajili ya kuwashukuru wananchi, pamoja na kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi. Akiwa katika kijiji cha Ngokolo, amesema baada ya kupata taarifa katika mkutano huo kuwa Zahanati ya kijiji hicho haina nyumba ya Mganga, na wananchi wamekuwa wakipata shida ya kupata matibabu hasa nyakati za usiku…