AZANIA BANK TAWI LA KIBAHA YALETA MATUMAINI MAKUBWA KUPITIA MPANGO WA FANIKISHA MWANAMKE HODARI
AZANIA BANK TAWI LA KIBAHA YALETA MATUMAINI MAKUBWA KUPITIA MPANGO WA FANIKISHA MWANAMKE HODARI
Na Victor Masangu, Kibaha Katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwakomboa wanawake katika kujikwamua kiuchumi Azania bank imeamua kuja na mpango kabambe uliopewa jina la Fanikisha Mwanamke Hodari ambao utaweza kuwasaidia kupata mikopo yenye riba nafuu ambayo itawasaidia kiasi kikubwa kuendesha shughuli zao na kujiingizia kipato lengo ikiwa ni kuodokana na wimbi la umasikini na kujikwamua kiuchumi. Hayo yamebainisha na Meneja wa Azania bank tawi la Kibaha mjini Anna Monyo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na baadhi ya wanawake kutoka kata mbali mbali za Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha kwa lengo la kuweza kuwapatia elimu na mafunzo mbali mbali yanayohusiana na fursa zilizopo ikiwa pamoja na jinsi ya kutumia mkopo ambao wanautoa wenye riba nafuu ya asilimia 1 kwa kipindi cha mwezi mmoja. Meneja huyo amebainisha kwamba lengo kubwa na mikakati ambayo wamejiwekea ni kuhakikisha kwamba wanamwezesha mwanamke kwa kumpatia mikopo ili a…