ANNA KILANGO: SAME MASHARIKI INAHITAJI BARABARA YA LAMI KISIWANI–MKOMAZI
ANNA KILANGO: SAME MASHARIKI INAHITAJI BARABARA YA LAMI KISIWANI–MKOMAZI
SAME MBUNGE wa Jimbo la Same Mashariki, Anna Kilango Malecela, amesema kuwa ili jimbo hilo liweze kukuza uchumi wake, ni muhimu Serikali kukamilisha ujenzi wa barabara ya Kisiwani–Mkomazi kwa kiwango cha lami. Kilango aliyasema hayo leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Soko la Kariakoo, Kata ya Ndungu, wilayani Same, wakati akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Aggrey Mwanri. Alisema kuwa amekuwa akiwasilisha ombi la ujenzi wa barabara hiyo kwa Serikali tangu mwaka 2000, alipokuwa Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, na kwamba juhudi hizo zimezaa matunda baada ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuipitisha barabara hiyo kujengwa kwa kiwango cha lami. “Kwa sasa mkandarasi mmoja amepewa fedha kidogo kidogo, lakini sasa amepewa Sh bilioni 1.5 na ameanza kwa nguvu kuijenga barabara hii kwa kiwango cha lami,” alisema Kilango. Aliongeza kuwa ataendelea kuisimamia kwa karibu kutokana na kuwa miongoni mwa wajumbe wa Kamat…