WMA DODOMA YAENDELEA KUTOA ELIMU NA KUKAGUA USAHIHI WA MASHINE ZA KUUZIA MAJI NA VIFAA VYA MAZOEZI (GYM)

WMA DODOMA YAENDELEA KUTOA ELIMU NA KUKAGUA USAHIHI WA MASHINE ZA KUUZIA MAJI NA VIFAA VYA MAZOEZI (GYM)
Dodoma - WMA Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Dodoma, Bw. Said Ibrahim, ameendelea na ziara ya kutoa elimu kwa wafanyabiashara pamoja na kukagua vipimo vinavyotumika katika biashara ya kuuza maji ya kunywa mtaani na vile vinavyotumika kwenye kumbi za mazoezi (Gym) jijini Dodoma tarehe 11 Agosti, 2026. Katika ziara hiyo, Bw. Said ametembelea maeneo mbalimbali yanayofanya biashara hizo, ikiwemo Makole, Makulu, Hazina, Wajenzi, Maili Mbili, Nkuhungu na Nyerere Square, kwa lengo la kujiridhisha kuwa vipimo vinavyotumika maeneo hayo vimehakikiwa na WMA. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Bw. Said amesema ukaguzi huo unaenda sambamba na utoaji wa elimu kwa wafanyabiashara kuhusu umuhimu wa kutumia vipimo sahihi na vinavyokidhi vigezo. Amesema WMA imejiridhisha kuwa mashine za kuuza maji ya kunywa zilizotembelewa zinatoa vipimo sahihi kulingana na thamani ya fedha aliyotoa na ujazo wa maji ambao anauhitaji. Aidha, katika kumbi za mazoezi, WMA imekagua vifaa mbalimbali vinavyohusiana na uzi…