Wenye uzito uliopitilizwa waitwa kufanyiwa matibabu

Wenye uzito uliopitilizwa waitwa kufanyiwa matibabu
*Kambi maalum inaanza Jumatatu hadi Septemba 11 Na Mwandishi Wetu HOSPITALI ya Shifaa Pan African ya Kinondoni jijini Dar es Salaam imeandaa kambi maalum kufanya upasuaji wa kupunguza uzito kwa kutumia matundu madogo kuanzia Agosti 31 mpaka Septemba 11.  Daktari bingwa wa upasuaji wa hospitali hiyo, Kassim Bahsan alisema jana kuwa kambi hiyo itafanyika katika hospitali hiyo kuanzia Agosti 31 mwezi huu hadi Septemba 11. Alisema katika kambi hiyo wananchi watapata fursa ya kufanyiwa tathmini ya mwili na kupata ushauri wa kitaalamu wa upasuaji wa kupunguza uzito kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya matundu madogo. “Kama umekuwa ukipambana na unene kupita kiasi na unatafuta njia salama na yenye ufanisi ya kuboresha afya yako hii ni fursa muhimu ya kuchukua hatua kuelekea maisha yenye afya bora,” alisema Dk Bahsan Alisema tarehe 4 mwezi Septemba hospitali ya Shifaa itaendesha mdahalo wa elimu kwa umma ambapo wananchi wote wanalikwa kushiriki kupata uelewa wa upasuaji wa kupunguza uzito. “Ni semina…