WAZIRI MKUU AISIFU TADB KWA KUCHOCHEA MAPINDUZI YA KILIMO

WAZIRI MKUU AISIFU TADB KWA KUCHOCHEA MAPINDUZI YA KILIMO
Na Dotto Kwilasa, Dodoma Waziri Mkuu ameipongeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa mchango wake katika kuimarisha sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi nchini, huku akiitaka kuongeza uwezo wa kifedha ili kuwafikia wakulima wengi zaidi na kuharakisha mageuzi ya uzalishaji wa chakula na mazao ya biashara. Akizungumza baada ya kutembelea banda la TADB katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma, Waziri Mkuu amesema uwekezaji wa benki hiyo umeendelea kuongeza uzalishaji wa mazao, kuimarisha usalama wa chakula na kuinua kipato cha wananchi kupitia upatikanaji wa mitaji kwa wakulima, wafugaji na wavuvi. Amesema Serikali inahitaji kuona TADB ikijengewa uwezo mkubwa zaidi wa kifedha ili iwe chanzo cha uhakika cha mitaji kwa sekta ya kilimo, akibainisha kuwa utegemezi wa ruzuku pekee hauwezi kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya wakulima nchini. "Wakulima wanahitaji taasisi imara ya fedha itakayowawezesha kupata mikopo ya kununua mbolea, pembejeo na kuwekeza katika uzalisha…