WALIMU WA TANGA WAPEWA SILAHA MPYA ZA KUINUA UFAULU

WALIMU WA TANGA WAPEWA SILAHA MPYA ZA KUINUA UFAULU
WALIMU 328 kutoka shule 10 za Sekondari katika Jiji la Tanga wanapigwa msasa kupitia semina maalumu inayolenga kuwaongezea ujuzi na mbinu za ufundishaji, hatua inayolenga kuongeza ufaulu wa wanafunzi wa Kidato cha Pili na Nne. Semina hiyo inaendeshwa na Taasisi ya Tanzania Centre For Education kupitia mradi wa Tanga Yetu, unaofadhiliwa na Foundation Botnar na kutekelezwa kwa kushirikiana na Innovex, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kukuza ufaulu katika shule za Jiji la Tanga. Akizungumza wakati wa semina hiyo iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Nguvumali, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Centre for Education Yusuf Ogutu alisema mafunzo hayo ni mwendelezo wa semina zilizolenga kuwajengea uwezo walimu katika masomo mbalimbali. Alisema katika hatua hiyo walimu wa masomo ya Historia, Jiografia, Business Studies na Bookkeeping wamepatiwa mafunzo, huku awali semina ikiwa imefanyika katika Shule ya Sekondari Kihere kwa walimu wa Civics, Kiswahili, Kiingereza, Historia ya Tanzania na Maadili. O…