VYAMA SITA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYATAKIWA KUDUMISHA UMOJA NA MSHIKAMANO

VYAMA SITA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYATAKIWA KUDUMISHA UMOJA NA MSHIKAMANO
Na Victor Masangu,Kibaha VYAMA Sita Rafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika vimetakiwa kuendeleza ushirikiano ulioachwa na waasisi wa mataifa hayo ili kuleta maendeleo kwa wananchi. Hayo yamesemwa kwenye Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS) Kwa Mfipa Kibaha na Katibu Mkuu wa Chama cha SWAPO na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shule hiyo Sophia Shaningwa wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Programu hiyo. Shaningwa amesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia wakufunzi hao kuwajengea uwezo viongozi wa vyama hivyo tawala kwani wana nafasi kubwa ya kuleta maendeleo. Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Aggrey Mwanri ameipongeza shule hiyo kwa kuandaa mafunzo hayo kwa wakufunzi kwani yatasaidia kuleta maendeleo na kukuza uchumi. Mwanri amesema kuwa huo ni uwekezaji mzuri kwa viongozi ili kupata mbinu mbalimbali ikiwemo za mawsiliano na kuhudumia kwa usawa. Naye Mkurugenzi wa Masuala ya Kitaaluma na Wanafunzi wa Shule hiyo Profesa Ana Nhampule akielezea kuhusu mafunzo…