VIJANA WAPIGA DEBE MKATA WAVUNJA REKODI, WANUNUA COASTER KWA MKOPO WA HALMASHAURI

VIJANA WAPIGA DEBE MKATA WAVUNJA REKODI, WANUNUA COASTER KWA MKOPO WA HALMASHAURI
Na Mashaka Mhando, Handeni HATUA ya Serikali ya Awamu ya Sita kuwezesha makundi maalum kiuchumi imeanza kuzaa matunda makubwa Wilayani Handeni, baada ya kikundi cha vijana waliokuwa madereva, makondakta, na wapiga debe eneo la Mkata kufanikiwa kununua gari la abiria aina ya Toyota Coaster. Mafanikio hayo makubwa yamefikiwa kupitia mkopo wa Shilingi Milioni 90 utokanao na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa mwaka wa fedha 2025/2026. Taarifa ya mafanikio ya vijana hao imetolewa Leo Augosti 1, mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Tanga, wakiongozwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Bw. Mohammed Salim, waliokuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo. Akiwasilisha taarifa ya mradi huo unaomilikiwa na kikundi hicho cha vijana cha Mkata, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Saitoti Stephen, alisema mradi mzima unagharimu Shilingi Milioni 100.  Saitoti alifafanua kuwa, kati ya fedha hizo, Shilin…