VIJANA TANGA WABUNI TEKNOLOJIA YA KUWAOKOA WAVUVI Na Oscar Assenga, TANGA Programu ya Tanga Yetu imeendelea kuwa chachu ya maendeleo kwa vijana na watoto wa Jiji la Tanga, kupitia miradi inayolenga kuimarisha elimu, ujuzi, teknolojia na ubunifu kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii. Akizungumza katika Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu, Afisa Mawasiliano wa Programu ya Tanga Yetu, Cliford Sangai, alisema programu hiyo inayofadhiliwa na Foundation Botnar na kutekelezwa na Kampuni ya Innovate kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Tanga, imeshiriki maonyesho hayo kuonyesha matokeo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa jijini humo. Alisema Tanga Yetu inatekeleza zaidi ya miradi 15 katika maeneo ya elimu, teknolojia na ubunifu, ikiwa na lengo la kuhakikisha watoto na vijana wanapata fursa za kukuza uwezo wao na kutumia maarifa kutatua changamoto zinazowakabili. “Tumekuja kwenye wiki hii kuonyesha namna ambavyo Tanga Yetu imekuwa ikifadhili miradi mbalimbali katika elimu, ujuzi na ubunifu, pamoja na kuonyesh…