USHIRIKIANO WA NHIF NA ZHSF WAVUTIA KAMATI YA BAJETI YA BARAZA LA WAWAKILISHI

USHIRIKIANO WA NHIF NA ZHSF WAVUTIA KAMATI YA BAJETI YA BARAZA LA WAWAKILISHI
Na Mwandishi Wetu, Dodoma Kamati ya Bajeti ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar imeupongeza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kazi kubwa inayofanya katika kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma za bima ya afya nchini, pamoja na ushirikiano wake na Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF). Pongezi hizo zimetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Mariam Hamis Said, wakati Kamati hiyo pamoja na Menejimenti za ZHSF na NHIF ilipotembelea Makao Makuu ya NHIF kwa ajili ya kujifunza namna Mfuko huo unavyoendesha na kutoa huduma kwa wanachama. Mhe. Mariam amesema ziara hiyo imekuwa na mafanikio makubwa, kwa kuwa Kamati imepata fursa ya kuelezwa na kujionea kwa vitendo mifumo na huduma zinazotolewa na NHIF, kupitia ziara kwenye Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH). Pamoja na kutoa pongezi kwa NHIF, Kamati hiyo ilipata fursa ya kutaka kufahamu kwa kina masuala mbalimbali yanayohusu uendeshaji na maendeleo ya Mfuko, ikiwemo namna N…