TREY SONGZ NA DIAMOND PLATNUMZ WAKIWASHA JUKWAA LA IMBEJU SAUTI MOJA

TREY SONGZ NA DIAMOND PLATNUMZ WAKIWASHA JUKWAA LA IMBEJU SAUTI MOJA
DAR ES SALAAM: Usiku wa Tamasha la Imbeju Sauti Moja, lililoandaliwa na CRDB Foundation, umeacha gumzo kubwa kwa mashabiki wa burudani baada ya nyota wa muziki kutoka Marekani, Trey Songz, kuamua kumualika staa wa Tanzania, Diamond Platnumz, jukwaani. Tamasha hilo lililofanyika katika viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, liliwakutanisha mashabiki wa muziki waliojitokeza kwa wingi kushuhudia burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania. Hata hivyo, ujio wa Trey Songz ulikuwa miongoni mwa matukio yaliyotikisa zaidi usiku huo. Msanii huyo aliwasha jukwaa kwa vibao vyake maarufu kabla ya kumshangaza umati kwa kumkaribisha Diamond Platnumz. Mara tu Diamond alipotokea jukwaani, shangwe na mayowe vilitawala eneo hilo, huku mashabiki wakifurahia kuwaona mastaa hao wawili wakishirikiana mbele yao. Kilele cha burudani hiyo kilikuwa pale Trey Songz na Diamond Platnumz walipotumbuiza kwa pamoja wimbo wao mpya, ambao uliwasilishwa mbele ya mashabiki kwa mara ya kw…