TBS YAWAFUNGULIA WAJASIRIAMALI NJIA YA MASOKO KUPITIA UBORA WA BIDHAA
TBS YAWAFUNGULIA WAJASIRIAMALI NJIA YA MASOKO KUPITIA UBORA WA BIDHAA
Wajasiriamali na wananchi wanaoshiriki Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kusini wamepata elimu kuhusu umuhimu wa kuzingatia viwango, kuthibitisha bidhaa na kutumia Alama ya Ubora ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS), hatua inayolenga kuongeza uaminifu wa bidhaa na kufungua fursa zaidi za masoko ndani na nje ya nchi. Elimu hiyo imetolewa na TBS Kanda ya Kusini kupitia ushiriki wake katika Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika katika Viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi, ambapo wananchi na wajasiriamali wamepata fursa ya kupata ufafanuzi wa moja kwa moja kuhusu viwango, ubora na taratibu za uthibitishaji wa bidhaa. Akizungumza katika maonesho hayo, Meneja wa TBS Kanda ya Kusini, Abel Mwakasonda, amesema ushiriki wa shirika hilo ni sehemu ya juhudi za kuwafikia wananchi na kuwapatia elimu itakayowawezesha kuboresha bidhaa zao na kuongeza ushindani katika masoko. Amesema TBS imeendelea kuweka mkazo katika kuhakikisha wazalishaji, hususan wajasiriamali wadogo na wa kati, wanaelewa umuhimu wa kuthibiti…