TANZANIA KUWA KITOVU CHA UCHAKATAJI WA MADINI TEMBO

TANZANIA KUWA KITOVU CHA UCHAKATAJI WA MADINI TEMBO
Dkt.Kiruswa Ataka Ujenzi Kuharakishwa, Asisitiza Uongezaji Thamani Nchini Tayari WanaKigamboni 278 Wameajiriwa, Zaidi ya Asilimia 90 ni Watanzania *Mwezi Julai Pekee Mkoa wa Kimadini Dar/Pwani Umekusanya Bil 4.06* 📍 Kigamboni,Dar Es Salaam Tanzania imeingia katika Hatua Mpya ya Uendelezaji wa Madini Tembo (Heavy Mineral Sands), huku shughuli za uchimbaji zikiendelea kupitia Mradi wa Fungoni- Kigamboni na Tajiri sambamba na ujenzi wa Kiwanda cha Uchakataji wa Madini hayo Mkoani Tanga. Uchimbaji na uchakataji wa Madini Tembo unatekelezwa kupitia Kampuni ya Ubia ya Nyati Mineral Sands Limited, ambapo Serikali inamiliki hisa zisizofifishwa za asilimia 16. Akizungumza leo, Agosti 18, 2026, alipotembelea na kukagua shughuli za uzalishaji wa madini hayo katika Mradi wa Fungoni- Kigamboni, pamoja na kupata taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha uchakataji Tajiri- Tanga, Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, ameitaka kampuni hiyo kuharakisha ujenzi wa kiwanda hicho, akisisitiza dhamir…