TANESCO, POLISI DODOMA WAAHIDI KUIMARISHA USHIRIKIANO ULINZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME.
TANESCO, POLISI DODOMA WAAHIDI KUIMARISHA USHIRIKIANO ULINZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME.
Na Belinda Joseph-Dodoma. Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma limefanya kikao kikao kazi na Maafisa wa Jeshi la Polisi ngazi ya kata, wilaya na Mkoa wa Dodoma, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika ulinzi wa miundombinu ya umeme na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kulinda miundombinu hiyo. Akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Kurwa Mangara, amesema ushirikishwaji wa vyombo vya ulinzi ni muhimu kutokana na nafasi ya umeme katika maisha ya wananchi na shughuli za kiuchumi. Amesema hatua hiyo imechukuliwa kutokana na changamoto za uhujumu na uharibifu wa miundombinu ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme, ikiwemo wizi wa vyuma na bolti pamoja na uvamizi wa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya njia za kusafirisha umeme. Mangara ameeleza kuwa baadhi ya maeneo hayo yamekuwa yakitumika kwa shughuli za kilimo na uchimbaji wa mchanga na kokoto, hali inayoweza kusababisha mmomonyoko wa udongo na kuhatarisha nguzo pamo…