TAMASHA LA UTAMADUNI LATUMIKA KUFUNGAMANISHA UCHUMI, KUENDELEZA URITHI WA WATANZANIA
TAMASHA LA UTAMADUNI LATUMIKA KUFUNGAMANISHA UCHUMI, KUENDELEZA URITHI WA WATANZANIA
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO MOROGORO: Tamasha la Nne la Kitaifa la Utamaduni linalotarajiwa kufanyika mkoani Morogoro kuanzia Agosti 25 hadi 29, 2026, limeelezwa kuwa ni nyenzo muhimu ya kufungamanisha utamaduni na uchumi, huku likilenga kuhifadhi, kuendeleza na kutangaza urithi wa Watanzania. Tamasha hilo pia linalenga kuimarisha utambulisho wa Taifa na historia yake kwa vizazi vya sasa na vijavyo, pamoja na kutoa fursa kwa wananchi kutumia utamaduni, sanaa na ubunifu kama chanzo cha ajira na kipato. Akizungumza Agosti 23, 2026 mbele ya waandishi wa habari katika Kambi ya Wapigania Uhuru Mazimbu, Morogoro, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema kufanyika kwa tamasha hilo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya Serikali ya kulinda na kuendeleza utamaduni wa Mtanzania. Amesema utamaduni unapaswa kutumika kujenga maadili, kuimarisha utaifa na mshikamano, kukuza uchumi bunifu, kuongeza fursa za ajira na biashara, pam…