TAEC YAWEKA MIKAKATI YA USALAMA WA NYUKLIA KWA AFCON 2027
TAEC YAWEKA MIKAKATI YA USALAMA WA NYUKLIA KWA AFCON 2027 Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), kwa kushirikiana na Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomu (IAEA), imeanza kuimarisha maandalizi ya usalama wa nyuklia na mionzi kuelekea Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, ambazo Tanzania itakuwa mwenyeji kwa pamoja na Kenya na Uganda. Maandalizi hayo yanalenga kujenga uwezo wa kitaifa wa kuzuia, kubaini na kukabiliana na vitisho vinavyoweza kuhusisha nyenzo za nyuklia au vyanzo vingine vya mionzi wakati wa mashindano hayo, ambayo yanatarajiwa kuvutia wachezaji, viongozi, mashabiki, waandishi wa habari na wageni kutoka mataifa mbalimbali. Akifungua rasmi jijini Arusha warsha ya siku tano kuhusu uandaaji na utekelezaji wa hatua za usalama wa nyuklia katika matukio makubwa ya umma, Mkurugenzi Mkuu wa TAEC, Profesa Najat Kassim Mohammed, amesema ukubwa na hadhi ya AFCON 2027 vinahitaji maandalizi ya kina na ushirikiano wa taasisi mbalimbali ili kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika katika mazingira salama. Warsha hiyo, inayofanyika …