STANBIC YAHIMIZA UFADHILI UNAONGOZWA NA WAAFRIKA ILI KUFUNGUA FURSA ZA MIUNDOMBINU BARANI AFRIKA
STANBIC YAHIMIZA UFADHILI UNAONGOZWA NA WAAFRIKA ILI KUFUNGUA FURSA ZA MIUNDOMBINU BARANI AFRIKA
Afrika inapaswa kutumia zaidi mitaji yake ya ndani, kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kukuza masoko ya fedha ya ndani ili kuziba pengo la ufadhili wa miundombinu na kuchochea ukuaji wa uchumi wa muda mrefu, Benki ya Stanbic Tanzania imesema. Kauli hiyo ilitolewa wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanahisa wa Africa50 na Jukwaa la Miundombinu la Afrika (Africa Infrastructure Forum), lililofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam, likiwakutanisha viongozi wa kisiasa, wataalamu wa masuala ya fedha na maendeleo kujadili namna taasisi za Afrika zinavyoweza kushirikiana kufadhili maendeleo ya bara, wakati ambapo uwekezaji wa kimataifa unazidi kuwa wa kuchagua. Akizungumza katika kikao cha mjadala kilichokuwa na mada “Pace Setters: African-Designed, African-Led” (Waongoza Njia: Yaliyobuniwa na Kuongozwa na Waafrika), Mkurugenzi Mtendaji wa Stanbic Bank Tanzania, Manzi Rwegasira, alisema Afrika tayari ina taasisi imara za kifedha, lakini kinachohitajika sasa ni kuongeza uwezo wa taasisi h…