STAMICO YASAINI MKATABA MNONO NA CHUO CHA MAFUNZO (ZANZIBAR )ZNZ
STAMICO YASAINI MKATABA MNONO NA CHUO CHA MAFUNZO (ZANZIBAR )ZNZ
Shirika la Madini la Taifa ( STAMICO) katika muendelezo wa kuhakikisha linaendelea kuwa kinara katika kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi Tanzania nzima, leo tarehe 11/8/2026 imeingia mkataba mnono wa pande tatu kati ya STAMICO, Chuo cha Mafunzo na taasisi ya FDH ya kuhakikisha magereza yote ya Zanzibar yanaanza kutumia Nishati ya Rafiki Briquettes. Makubaliano hayo yamefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar na kushuhudiwa na Kamishna wa Magereza Zanzibar Khamis Abdalah Khamis pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt Venance Mwasse na Mkurugenzi wa FDH Bwn Michael Salali. Akiongea katika hafla hiyo, Dkt Mwasse ameipongeza taasisi ya FDH kwa kufanikisha kuingia makubaliano haya ambayo yatawezesha Magereza zote za Zanzibar kupata Nishati hii ya Rafiki Briquettes ambayo inaenda kuleta afueni kwenye gharama za Nishati kwa Magereza lakini pia kuanza kutekeleza agenda ya Nishati Safi kwa taasisi zote zinazohudumia watu zaidi ya 100. "Suala la…