Shule Binafsi, Serikali Zahimizwa Kuimarisha Ushirikiano wa Kielimu na Kijamii
Shule Binafsi, Serikali Zahimizwa Kuimarisha Ushirikiano wa Kielimu na Kijamii
Shule zinazomilikiwa na taasisi na wawekezaji binafsi zimetakiwa kuimarisha ushirikiano wa kitaaluma na kijamii baina yao pamoja na shule za Serikali, huku zikitumia ushindani wa kiushindani kama chachu ya kuboresha viwango vya elimu na kukuza maendeleo ya wanafunzi. Wito huo umetolewa na Diwani wa Kata ya Kwembe katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Kawina Hadji Konde, alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya saba ya Shule ya Awali na Msingi ya Mwendo, iliyopo Kibamba kwa Mangi, wilayani Ubungo. Akizungumza katika hafla hiyo iliyowakutanisha wazazi, walimu, wanafunzi na wadau mbalimbali wa elimu, Bw. Konde alisema shule binafsi na zile za Serikali zina nafasi kubwa ya kujenga mifumo ya ushirikiano katika maeneo mbalimbali, ikiwemo elimu, michezo, sanaa, utamaduni na shughuli za kijamii, kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kuinua viwango vya elimu kwa manufaa ya wanafunzi na jamii kwa ujumla. Alisema ushindani kati ya shule unapaswa kujengwa katika misingi…