SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA MABARAZA YA ARDHI
Na Munir Shemweta, Dodoma Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imekutana leo tarehe 12 Agosti 2026 Bungeni jijini Dodoma kupokea na kujadili taarifa kuhusu utendaji wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya, ikiwa ni sehemu ya jukumu la Bunge la kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa majukumu ya Serikali katika sekta ya ardhi. Katika kikao hicho, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeieleza Kamati hatua mbalimbali zilizochukuliwa katika kuboresha utendaji wa Mabaraza hayo, ambayo yako chini ya Wizara hiyo. Miongoni mwa hatua zilizobainishwa ni kuongezeka kwa idadi ya Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya, kupungua kwa mashauri na malalamiko, kuimarishwa kwa matumizi ya mifumo ya kidijiti pamoja na kuboreshwa kwa mfumo wa uendeshaji wa shughuli za madalali. Pamoja na mafanikio hayo, Kamati imeelezwa kuwa bado zipo changamoto kadhaa zinazoathiri utendaji wa Mabaraza hayo na kwamba Wizara inaendelea kuzifanyia kazi ili kuongeza ufanisi na kuboresha utoaji wa hudu…