SELF MF YATOA FURSA ZA MIKOPO YA KILIMO NA BIMA ZA MAZAO MAONESHO YA NANENANE

SELF MF YATOA FURSA ZA MIKOPO YA KILIMO NA BIMA ZA MAZAO MAONESHO YA NANENANE
Mfuko wa SELF (SELF MF) umezitaka wananchi, hususan wakulima na vijana, kutumia fursa za mikopo nafuu zinazotolewa na taasisi hiyo ili kuwekeza katika shughuli za kilimo, kuongeza thamani ya mazao na kujikwamua kiuchumi. Akizungumza katika Maonesho ya Kimataifa ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, Meneja wa Soko na Uhamasishaji wa SELF MF, Linda Mshana, amesema taasisi hiyo iliyo chini ya Wizara ya Fedha imejikita katika kutoa huduma za kifedha zenye masharti nafuu kwa wananchi, huku sekta ya kilimo ikiwa miongoni mwa maeneo yenye kipaumbele. Mshana amesema SELF MF inatoa mikopo inayogusa mnyororo mzima wa thamani wa kilimo kuanzia uzalishaji, uchakataji, usafirishaji, kuongeza thamani ya mazao hadi bidhaa kumfikia mlaji. “Tumekuja kuwaonyesha wananchi kuwa kuna fursa nyingi za mikopo katika sekta ya kilimo. Tunafadhili shughuli zote katika mnyororo wa thamani wa kilimo ili kuwasaidia wakulima na wajasiriamali kukuza biashara zao,” amesema Mshana. Amesema ta…