SEIF GULAMALI;KIELELEZO CHA UONGOZI WA HEKIMA NA UPENDO KWA JAMII
SEIF GULAMALI;KIELELEZO CHA UONGOZI WA HEKIMA NA UPENDO KWA JAMII
Aliiongoza Manonga kwa weledi mkubwa, ‘figisu’ ujumbe Kamati Utendaji Yanga wamtoa uongozini Na Mwandishi Wetu KATIKA Jamii yoyote, viongozi bora ni wale wanaotambua kwamba mafanikio ya kweli hupimwa kwa mchango wao katika kuboresha maisha ya wengine kwa namna moja au nyingine. Miongoni mwa watu wanaotajwa kwa sifa nzuri za uongozi unaojengwa juu ya maadili, uwajibikaji na upendo kwa jamii ni pamoja na Seif Gulamali, kijana mpole ambaye amewahi kuliongoza Jimbo la Manonga kwa kipindi Cha awamu mbili tofauti, akitimiza majukumu yake ya kuwatumikia wananchi. Kwa wasiomfahamu Gulamali, sifa yake kubwa ni uwezo wa kuwasikiliza watu na kuthamini mawazo yao bila ubaguzi wa aina yoyote na zaidi akiwa kiongozi aliyejijengea tabia ya kuwa msikilizaji wa masuala mbalimbali ya kijamii na hasa yale yanayogusa maisha ya watu. Kupitia mwenendo wake, Seif Gulamali ameonyesha kuwa uongozi si mamlaka pekee, bali ni huduma kwa watu na kujitoa kwa ajili ya manufaa ya wengi pasipo kuwabagua kwa namna moja au …